Mwenye heri

Mwenye heri ni jina la heshima analopewa Mkristo wa Kanisa Katoliki baada ya kufa na ya kufanyiwa kesi makini kuhusu sifa ya utakatifu alilonalo.
Vigezo
[hariri | hariri chanzo]Kwa mfiadini inatosha kushuhudia kwa hakika kwamba aliuawa kwa ajili ya imani au adili lingine [1].
Kwa Wakatoliki wengine unatakiwa ushujaa wa maadili yake yote, hasa yale ya Kimungu na maadili bawaba, sala na unyenyekevu.
Mwaka 2017 Papa Fransisko aliongeza uwezekano wa mtu kutangazwa mwenye heri kutokana na tendo la kishujaa la kuhatarisha uhai wake na kufupisha maisha yake kwa sababu ya upendo.
Njia hizo mbili za mwisho zinatakiwa kuthibitishwa na muujiza mmoja [2][3][4] uliofanywa na Mungu kwa maombezi ya mtumishi wake baada ya kifo chake.
Asili ya hatua hiyo ni karne XIV ambapo Papa alianza kukubali marehemu aheshimiwe kwa namna ya pekee mahali fulani au katika shirika fulani kabla kesi ya kumtangaza mtakatifu kwa Kanisa lote haijakamilika. Hata hivyo tarehe 6 Julai 1634 Papa Urban VIII aliuwekea Ukulu mtakatifu tu mamlaka ya kumtangaza mwenye heri mpya[5][6].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Sarno, Robert J., "Process of Canonization", Archdiocese of Oklahoma City". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Juni 2018. Iliwekwa mnamo 5 Juni 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ghose, Tia (9 Julai 2013). "The Science of Miracles: How the Vatican Decides". livescience.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-09-15.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Miracles under the microscope". The Economist. 2000-04-20. ISSN 0013-0613. Iliwekwa mnamo 2019-09-15.
- ↑ Gjelten, Tom (31 Agosti 2016). "How The Catholic Church Documented Mother Teresa's 2 Miracles". NPR (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-09-15.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ A. De Meester, Juris Canonici et Juris Canonico-Civilis Compendium Nova Editio, Tomus Tertius, Pars Secunda (Brugis: Desclée de Brouwer et Sii, 1928) p. 86 (citing the canonist Pope Benedict XIV, De Servorum Dei Beatificatione et Beatorum Canonizatione)
- ↑ Beccari, Camillo (1907). "Beatification and Canonization." The Catholic Encyclopedia. Vol. 2. New York: Robert Appleton Company. Via New Advent. newadvent.org. Accessed 1 November 2015.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Beccari, Camillo (1907). "Beatification and Canonization". Catholic Encyclopedia. Robert Appleton Company. Vol. 2 – kutoka New Advent. newadvent.org.
Beccari, Camillo (1913). . Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company.- De Meester, A., J.C.D., Juris Canonici et Juris Canonico-Civilis Compendium Nova Editio, Tomus Tertius, Pars Secunda (Brugis: Desclée de Brouwer et Sii, 1928)
- Saunders, Rev. William (2003). "The Process of Becoming a Saint". Reprinted from Arlington Catholic Herald. Via Catholic Education Resource Center. catholiceducation.org.
- Vatican website, with new procedures
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- List of all Blesseds in the Catholic Church Archived 4 Februari 2014 at the Wayback Machine by GCatholic.org.
| Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwenye heri kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |